Watu 10 wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea katika barabara ya Nakuru- Eldoret kati ya basi la abiria la Green Line na lori ya mizigo.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana leo Jumapili, Februari 17 katika eneo la kwa Harun, Kamara Nakuru.
Akithibitisha tukio hilo, chifu wa kata ya Kamara Joseph Korir alieleza kuwa watu wanane walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki hospitalini walikokuwa wakipata matibabu.
Madereva wa magari hayo mawili ni kati ya waliofariki kufuatia ajali hiyo.
Jumla ya watu 74 waliohusika katika ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali za Molo na Koibatek kwa matibabu.
Wanafunzi waliofunga shule kwa likizo fupi ni kati ya waliojeruhiwa katika ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea siku moja tu baada ya ajali nyingine mbaya kufanyika katika barabara ya Kericho - Nakur.u eneo la Chepsir ambako watu watano walipoteza maisha.
Wakenya wamewalaumu vikali maafisa wa trafiki kwa ulegevu kazini ma kuutaka kama chanzo cha visa vya ajali ambavyo vimeonegezeka nchini.
Social Plugin