Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RPC ATAJA MAJINA YA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA HIACE, LORI NA PIKIPIKI BUKOBA


Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja watu waliopoteza maisha  katika ajali  ya  gari la mizigo aina ya Canter yenye namba za usajili T223 ATK gari la abiria aina ya Hiace lenye namba T 869 CHT na pikipiki iliyotokea jana usiku katika katika mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba.


 Amesema waliofariki katika ajali hiyo kuwa dereva wa lori Dickson Bakuza (25) na Niace Gervaz ambaye ni dereva wa Hiace inayomilikiwa na Huberth Ifunya.

Kamanda Malimi amewataja marehemu wengine kuwa ni Peter Ifunya (31) ambaye ni kondakta wa Hiace na mwendesha pikipiki Prudence Themistokres (30).

Amesema watu wanne waliofariki  ni wakazi wa Rwamishenye katika Manispaa ya Bukoba.

Aidha amewataja majeruhi wawili waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera kuwa ni Amir Mohamed 30) na Athanas Josephat (34) ambao hali zao zinaendelea vizuri. 

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Hiace na mwendesha pikipiki ambao walikuwa wakifuatana kutoka Mjini Bukoba kuelekea nje ya Mji na walipofika katika mlima Nyangoye eneo la Hamugembe, walijaribu kulipita Gari aina ya Noah bila uangalifu na kugongana uso kwa uso na Canter. 

Amesema baada ya kugongana Hiace iliwaka moto na kusababisha Canter nayo kushika na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog Bukoba
PAKUA APP YA MALUNDE1 BLOG HAPA MARA MOJA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com