Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba amepata ajali leo asubuhi Jumatano Februari 13, 2019 katika eneo la Migori mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani kupata ajali na kwamba amepelekwa katika hospitali ya Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Alphonce Chandika amesema walimpokea mbunge huyo saa 3:30 asubuhi.
"Alikuwa akilalamika maumivu katika nyonga, mguu wa kulia. Tumempeleka katika vipimo ikiwemo CT Scan," amesema.
Social Plugin