Habari za hivi punde kutoka Dodoma zinasema kikao cha Bunge kimesitishwa kwa muda baada ya alarm 'king'ora' kulia ghafla Bungeni leo asubuhi Jumanne Februari 5,2019.
Shughuli za Bunge zimelazimika kusimama kwa muda baada ya kutokea hali ya taharuki ndani ya ukumbi wa bunge, baada ya kulia king’ola kinachoashiria na hali ya hatari na kusababisha wabunge kutoka nje bila kufuata utaratibu.
Hali hiyo imetokea majira ya saa 10.58 wakati wa kipindi cha maswali na majibu muda mfupi baada ya Naibu Spika Dk.Tulia Akson kuuliza swali la Nyongeza kwa Naibu Waziri Maji na Umwagiliaji Jumaa Awesso na alipoanza kujibu ghafla king’ora kinachoashiria hatari kuanza kulia na kusababisha wabunge kuanza kupiga kelele na kukimbia kutoka ukumbi wa bunge na kwenda nje.
Kutokana na hali hiyo wabunge walianza kupiga kelele kwa kusema kuwa hatari, hatari na bila kufuata utaratibu unaotakiwa na kusababisha Mwenyekiti wa Bunge, Najima Giga kutangaza kuhairisha shughuli za Bunge.
Bado haijaeleweka kuwa nini kilisababisha kulia kwa king’ola hicho kinachoashiria uwepo na hali ya hatari, lakini baada muda wavunge wamerudi bungeni kuendelea na kikao hicho.
Hii ni mara ya pili kutokea kwa hali ya sintofahamu ndani ya ukumbi wa Bunge kwani wiki mbili zilizopita kulitokea mtafuruku baada ya kuingia bundi ndani ya bunge jambo ambalo halijawahi kutokea tangu kujengwa kwa ukumbi huo.
Pamoja na kutokea kwa bundi ndani ya ukumbi Spika wa Bunge alisema kuwa Bundi wa Mchana hana shida ila bundi wa usiku ndiye mwenye kuleta tatizo.
Via Mwanahalisionline