Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: BALOZI SEIF ALI IDD AUNGURUMA SHINYANGA MJINI..AWATAKA WANA CCM KUACHANA NA SIASA ZA MAKUNDI

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga amehutubia mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika.



Mkutano huo ambao ni sehemu ya kusherekea miaka 42 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi umefanyika leo Jumatano Februari 13,2019 katika Viwanja vya Zimamoto vilivyopo Mjini Shinyanga.


Akihutubia mkutano huo amewataka wanaCCM kuwa na umoja,kushirikiana na kuacha siasa za  makundi kwani makundi yanagawa chama.

“Tushirikiane,tushikamane ili chama chetu kiwe imara na tuweze kushinda kwenye uchaguzi,nawasihi muache siasa za makundi”,amesema Balozi Idd.

Ametumia fursa hiyo kuwapongeza wabunge wote wa CCM mkoa wa Shinyanga kwa michango mbalimbali wanayotoa katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga akizungumza

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika akimpatia taarifa ya jimbo la Shinyanga Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga 

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika akizungumza

Mheshimiwa Masele akizungumza









Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Bi Asha akiwasalimia wakazi wa Shinyanga











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com