Ndugu wanahabari na watanzania wote, bila shaka mmemsikia Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai tarehe 31 /01/2019 akitoa taarifa bungeni au kile alichakuwa akikiita kuwa ni ufafanuzi juu ya malalamika ya malipo ya matibabu ya Mh Tundu Lissu (MB) wa Singida Mashariki na Mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
CHADEMA tunalazimika kumjibu Spika Ndugai kwa kuwa bila haya na kwa makusudi ameamua kuliongopea Bunge na umma wa Watanzania. Mh Tundu Lissu ametibiwa na Chama chake CHADEMA, wanachama mmoja mmoja,mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, watanzania waishio ndani na nje na sambamba na hilo wabunge mmoja mmoja walichangia takribani Tsh 43 millioni kutoka katika posha zao kama walivyofanya watanzinia wengine.
Mh Lissu ni Mbunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria ya bunge anastahili kulipwa mshahara wake wa kibunge na posha mbalimbali na pia kutibiwa na Bunge.
Takribani Tsh. 207 million alizopatiwa Mh Lissu ni stahikl zake halali za kibunge na si pesa ya Matibabu kama Spika alivyoliongopea bunge na umma wa Watanzania.
Spika amedai kuwa anazo nyaraka za uthibitisho wa malipo ya matibabu tunamtaka atoe hizo nyaraka hadharani .
Sisi Chama,Familia na Mh Lissu mwenyewe wote tuna nyaraka zote za Matibabu kwa kila hatua. Tunalitaka Bunge kulipia Matibabu ya Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa ni haki yake kisheria na si huruma kama anavyojaribu kuonyesha
Social Plugin