Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CiC-TZ NA UTPC ZAWAALIKA WAANDISHI WA HABARI KUCHANGAMKIA FURSA YA MRADI WA MIAKA MITATU



Shirika la Children in Crossfire (CiC-TZ) ni shirika la kimataifa la misaada lenye makao yake nchini Ireland ambalo kusudi la kuanzishwa kwake ni kusimamia haki na mahitaji ya watoto wadogo ambao wapo kwenye jamii maskini duniani.

CiC-TZ kupitia mradi wake wa kuongeza uelewa na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma bora za Malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (Early Childhood Development – ECD), limeingia makubaliano ya kimkakati ya miaka mitatu (2019 – 2021) na taasisi ya UTPC kupitia waandishi wa habari walioko kwenye klabu za waandishi wa habari nchini kote, kwa kuvishirikisha vyombo vya habari katika ngazi zote za mkoa na taifa.

Lengo maalumu la ushirikiano huu ni kuleta ufanisi kwa kuvishirikisha vyombo vya habari hasa katika ngazi ya mikoa na kitaifa kupitia UTPC na klabu zake katika kuimarisha na kuboresha uelewa na uwajibikaji katika eneo hili la malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (Early Childhood Development – ECD) ili kuwapa watoto nafasi ya kufikia uwezo wao kamili kwenye maisha.

Waandishi wote ambao ni wanachama wa klabu wanahimizwa kuomba maombi maalumu ya kushiriki kwenye mradi huu kama ambavyo maelekezo yalivyotolewa kwenye klabu za waandishi wa habari nchini kote.

Maombi yote yatumwe kwenye anuani ifuatayo. 
(Unashauriwa kutumia baruapepe)

Mkurugenzi Mtendaji
UNION OF TANZANIA PRESS CLUBS (UTPC)
S.L.P 314
Mwanza
Email: utpctz@yahoo.co.uk

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com