WASANII WATAJWA KUWA WAATHIRIKA NAMBA MOJA WA MADAWA YA KULEVYA

Mamlaka ya Kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya nchini imepanga kukutana na wasanii mbalimbali ili kuwapa elimu ya madhara ya dawa za kulevya ikiwa wao ni miongoni mwa wa waathirika wa dawa hizo kwa kutumia au kutumiwa kama wabebaji.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo kugundua kuwa wasanii ni waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya hivyo wamepanga kutoa vipeperushi vya kila aina ya dawa za kulevya vinavyoeleezea athari zake lengo ikiwa ni kufikisha taarifa kwa watu wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Rodgers Sianga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Jumatatu Februari 11, ambapo amesema wamepanga kukutana na wasanii hao Jumatano Februari 13 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Uingizwaji wa dawa nchini umepungua, tulipodhibiti nchi kavu walihamia katika njia za bahari ambapo kwa mwaka jana pekee tulikamata tani 9, 000 za dawa za kulevya zilizotaka kuingizwa nchini kwa njia ya majini na kwa nchi kavu tulikamata kilo 1, 000 za dawa kwa kushirikiana na majeshi ya majini bila hivyo hali yetu ingekuwa mbaya sana.

“ Kuhusu matumizi hatujajua yamepungua kiasi gani hivyo tunapanga mwishoni mwa mwaka huu kufanya tafiti ili tujue yamepungua kwa kiasi gani upatikanaji wake na matumzi yake kwa waathirika wa dawa ya kulevya na ndiyo sababu ya kuwaita wasanii ili watusaidie kufiklisha elimu kwa watu wengi” amesema.

Aidha Kamishna Sianga amesema wamejipanga kuhamishia nguvu katika mipaka ya Kusini ili kudhibiti uingizwaji wa dawa kutokea nchini Msumbiji kupitika katika ya mikoa ya kusini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post