Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa wa Tanga
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akizungumza katika mafunzo hayo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco akizungumza katika mafunzo hayo
Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt. Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
Msanii nguli wa Filamu mkoani Tanga akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kulia ni KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo kushoto ni nKATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco.
Wasanii wa filamu hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazingatia waledi na ufanisi mkubwa kwenye kazi zao ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii zinazowazunguka kutokana na tasnia hiyo hivi sasa kuwa mkombozi kwenye jamii.
Hayo yalisemwa na Mwezeshaji wa Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt. Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
Alisema sanaa inaweza kuwa tija kubwa ya maendeleo kwa wasanii kwa kutengeneza ajira nyingi na kuweza kuwakomboa iwapo wataizingatia na kuithamini kwa kuonyesha walezi kwenye kazi zao.
“Ndugu zangu wasanii labda niwaambie kwamba mkiwa makini kwenye kazi zenu na kuzingatia weledi mkubwa mnaweza kufika mbali kimafanikio kutokana na namna tasnia ya filamu hapa nchini iliyokuwa”,alisema.
Aidha alisema pia wasanii lazima watambue kwamba hawawezi kutengeneza filamu nzuri kama hawatakuwa na muda wa kutazama wenzao wanafanya nini kwani kupitia wenzao wanaweza kujifunza na kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa”,alisema.
“Labda pia niwaambie kwamba waledi kwenye kazi ya sanaa ni kitu muhimu sana inaweza kukupa maendelea makubwa kwa kuhakikisha mnaipenda na kuithamini",alisema.
Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo alisema sekta ya filamu ni ya kiuchumi kutoka Tanzania ni ya pili kwa idadi uzalishaji ukilinganisha na nchi ya Nigeria lakini ukija kwenye pato la taifa kidogo wanahitaji kuongeza nguvu.
Alisema bodi ya filamu imeweka mpango mahususi wa kuwajengea uwezo wadau wa filamu hapa nchini hususani kwenye maeneo ya kuboresha kazi zao ili ziwe kuwa na tija.
Aidha alisema hilo linatokana na baadhi ya wasanii hususani wanaochipukia kutokutambua namna ya kuweza kutengeneza kazi zao na kuweza kuzitangaza ili ziweze kuwa na manufaa makubwa kwao.
Social Plugin