Dada wa msanii Godzilla, Joyce Mbunda, amefunguka juu ya kile alichoambiwa na marehemu Godzila, wakati umauti ukimkuta.
Joyce amesema wakati umauti ukimkuta mdogo wake, yeye na mama yake walikuwa wamemshika baada ya kumuona anatapatapa, na ndipo alipomwambia dada yake asimuachie kwani kuna watu wanamfuata.
“Alinifuata chumbani kwangu akaniambia, sister naomba nilale hapa kidogo, maana kule kuna watu, watu wengi sana wananifuata, na mimi sitaki, nikamuacha alale
"Dakika kumi hazijafika akatoka ananiambia naenda nje, nikamwambia twende wote, mama akamshika na mimi nikamshika, tunamzuia atulie maana anahangaika, tulivyomshika analegea huku anakaa chini, alikuwa ananiambia cha tu sister, nimemshikilia hivi, namwambia niambie kitu, anashindwa hata kuzungumza, mpaka analegea yuko mikononi mwangu”, amesema Joyce.
Joyce ameendelea kwa kusema kwamba Godzilla alikuwa mtu mwenye upendo, na mtu ambaye alikuwa karibu sana na familia yake.
Godzila amefariki alfajiri ya leo baada ya kuzidiwa, kutokana na maradhi ya sukari na presha iliyokuwa ikimsumbua.
Social Plugin