Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema nchi yake imepania kutanua nguvu zake za kijeshi na mpango wake wa silaha za nyuklia licha ya shinikizo kutoka kwa nchi alizozitaja kuwa mahasimu zinazotaka kudhibiti uwezo wake wa kujihami.
Akiwahutubia maelfu ya watu waliojitokeza katika ukumbi wa Azadi mjini Tehran kuadhimisha miaka 40 tangu Mapinduzi ya Kiislamu, Rouhani amesema hawajawaomba yeyote wala hawataomba ruhusa kutengeza aina mbali mbali za makombora na wataendelea na njia yao ya kujiongeza nguvu za kijeshi.
Mamilioni ya watu wanahudhuria maadhimisho hayo ya miaka 40 tangu mapinduzi ya Kiislamu katika mji mkuu Tehran na miji mingine, siku inayokuchukuliwa kama ushindi wa mapinduzi yaliyoung'oa utawala wa Kifalme mnamo tarehe 11 Februari, 1979.
Chanzo:Dw