JKT TANZANIA YAICHARAZA USALAMA FC YA MANYARA 4 -0


Na Beatrice Mbise - Manyara

Timu ya mpira wa miguu ya JKT Tanzania inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara imeicharaza goli nne kwa sifuri timu ya Usalama FC ya mkoa wa Manyara ambayo inashiriki ligi daraja la pili.

Katika mchezo huo wa kirafiki ambao umechezwa leo katika uwanja wa shule ya Singe Sekondari ya mjini Babati mkoani Manyara Afisa Habari wa JKT Tanzania Jamillah Mutabazi ameeleza umuhimu wa wao kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kukutana na timu ya Singida United ya mkoani Singida.

"Katika mchezo huu sisi JKT Tanzania tumeibuka mshindi kwa kufunga goli nne kwa bila, lengo la kufanya mchezo huu kwanza kabisa ni kuweka ule ukaribu, urafiki na ujirani baina yetu sisi na wenzetu wa timu ya Usalama FC, ni mchezo wa kirafiki ambao kwetu sisi ni wa faida kwa sababu kwanza wachezaji wanakuwa wanapata nafasi ya kufahamiana na kujuana.

"Mchezo huu umetuweka sehemu nzuri kwa sababu licha ya kwamba tunaweka miili fiti kwa ajili ya mchezo unaofuata ambao ni wa 'FA' tunaoenda kucheza mjini Singida lakini jinsi ambavyo mchezo ulikuwa ni wa taff mchezo mzuri wa kasi kwa wachezaji umekuwa wa faida kwao kwa sababu siku zote mazoezi ukifanya mwenyewe unashindwa kujitathmini kwamba uko kwenye position gani, lakini ukipata mtu ambaye unaweza uka compit nae ni kitu ambacho kitakujenga zaidi", amesema Mutabazi.

Kwa upande wake Afisa Habari wa timu ya Usalama FC ya mkoani Manyara Elia Kimani amesema kuwa huo ni mchezo wa kirafiki ni mchezo ambao umekuja ghafla na walikuwa hawajajiandaa kama wangekuwa na mechi ambapo mechi ilikuwa ipigwe jana ghafla lakini haikuchezwa kwa hiyo sio mchezo ambao utasema unakatisha watu tamaa kwa kuwa sio wa ligi.

"Kwenye ligi tuna mwenendo sio mzuri sana na wala sio mbaya sana kwa sababu sisi sio moja ya timu ambazo zinaenda kushuka daraja, sisi tunaendelea kubaki ligi daraja la pili kwa mwenendo lakini tayari tunaweka mipango kwa ajili kujipanga kwa msimu ujao.

"Timu imecheza vizuri wachezaji wamejitahidi kadri ya uwezo lakini mzoefu ni mzoefu tu, wametuzidi kwenye uzoefu tu sioni kama wametuzi sana kwenye kiwango kwa sababu tulikuwa tumeshawakata baadhi ya sehemu kwa hiyo hakuna suala la kukata tamaa hapo",amesema.

Huu ni mwendelezo wa maandalizi ya mechi ambazo timu ya Usalama FC wanataraji kuzimalizia mechi za ligi daraja la pili katika ngwe ya mwisho ambayo wanaelekea kumaliza na mechi hizo mbili zitachezwa hapa mjini Babati. 

Kikosi cha JKT Tanzania kimetokea mkoani Tanga ambapo katika mchezo uliopita walimenyana na kikosi cha Yanga SC ambapo walipoteza mchezo huo kwa kukubali kichapo cha goli moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post