Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewasili Abuja, nchini Nigeria kuongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu nchini humo. Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 16 mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kikwete ameandika; "Nimewalisi Abuja, Nigeria kuongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Februari 2019 kufuatia ombi la Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. "
Social Plugin