Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MOTO WATEKETEZA GHALA LA KIWANDA CHA BORA


. Moja ya ghala la Kiwanda cha Bora jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto leo Alhamisi Februari 28, 2019.

Moto huo ulioanza saa 11 alfajiri umeteketeza ghala hilo kwa kiasi kikubwa lililopangishwa kwa ajili ya kuhifadhia vifaa vya ujenzi.

Kamanda wa Jeshi la Zima Moto Wilaya ya Temeke, Michael Bachubila amesema hadi sasa wamefanikiwa kuzima moto huo kwa asilimia 50 na jitihada zaidi zinaendelea.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com