Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NABII MAARUFU ATABIRI ATAUAWA KISHA KUFUFUKA BAADA YA SIKU TATU KAMA YESU


Nabii David Owuor
Nabii maarufu David Owuor ametabiri jinsi atakavyoondoka humu duniani baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa kufanya na Mungu. 


Owuor alisema muda wake umekaribia kufika ukingoni hapa duniani na Mungu amefurahishwa na kazi yake na kwamba kifo chake kitalinganisha na kile cha Yesu .

 Owuor ambaye hujitaja kuwa nabii mwenye nguvu zaidi ulimwenguni alisema ataondoka humu duniani jinsi Yesu alivyoondoka. 

Akitoa unabii kwa wafuasi wake katika kanisa la Repentance and Holiness Ministry, Owuor alisema alikutana na Mungu mawinguni na akamuelezea  habari ya kifo chake kwamba atauawa katika Mji wa Yerusalemu na mwili wake hautazikwa ila baada ya siku 3 atafufuka na kuenda mbinguni kukutana na Mungu. 

"Baba yangu na Mungu wangu amezungumza nami, alianza kuzungumza nami akiwa mwenye furaha kuu, aliniambia kwamba nitauawa pindi nitakapokamilisha kazi yake," Owuori alisema. 

 "Nitakufa kwa siku 3 na baada ya hapo nitafufuka na Mungu atanichukua kuenda mbinguni kulingana na kitabu cha Ufunuo 11:7.1," Owuor aliongeza.

 " Nitauawa baada ya kumaliza kufanya kazi ya Mungu, sitazikwa na kwa siku ya 3 Mungu atanichukua kuenda mbinguni, nitauawa Yerusalemu na hii sio mara ya kwanza mimi kuzungumza na Mungu, " Owuor aliongezea.

Picha za Owuor kwenye matukio mbalimbali

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com