Jamaa mwenye umri wa miaka 40 amelazwa katika hospitali ya Tharaka- Nithi nchini Kenya akiwa katika hali mbaya baada ya kujitahiri kwa wembe.
Katheya Riungu alijitahiri usiku wa Ijumaa, Januari 11 nyumbani kwake katika kijiji cha Mutunguni.
Habari kutoka kwa polisi zinaeleza kuwa wenyeji waliripoti kisa hicho kituoni jioni ya Jumapili Januari 13,2019 baada ya jamaa huyo kuvuja damu usiku kucha.
Riungu alichukua hatua hiyo baada ya kupata fununu kuwa rafiki zake walikuwa wamepanga kuthibitisha kama kweli ametahiriwa.
Kulingana na taarifa iliyondikishwa katika kituo cha polisi cha Chogoria, Riungu alipata fununu kuwa rafiki zake walikuwa wamepanga kuthibitisha kama kweli ametahiriwa.
Kwa kuogopa fedheha, aliamua kujitahiri kabla ya njama hiyo kutekelezwa.
"Walikuwa wamepanga tarahe ya kuthibitisha lakini Jumapili Januari 13, alikuwa amejitahiri kwa wembe na alikuwa akivuja damu,’’ ripoti hiyo.
Riungu alikimbizwa hadi katika hospitali ya ya rufaa ya Chuka anakoendelea na matibabu.
Social Plugin