Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, Amemuomba CAG kwenda kufanya ukaguzi maalum kwa fedha za ruzuku zilizotolewa na msajili wa vyama vya siasa kwa Lipumba na wenzake kwa kipindi chote ambacho walipata uhalali kutoka RITA.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Jumatatu muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kutengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) .
Amesema baada ya uamuzi huo wa mahakama ni vyema CAG, akafanya ukaguzi kwa kuwa bodi hiyo iliyokuwa kambi ya mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba haikuwa halali.
"Tumeupokea kwa furaha uamuzi huu wa Mahakama Kuu, umekata mzizi wa fitina wa madai yetu dhidi ya Rita. Nilishasema toka awali tutapokea uamuzi wowote wa mahakama utakaotolewa.
"Nawaomba wanachama wa CUF wawe watulivu kwa sasa wakati tukisubiri uamuzi mwingine utakaotolewa hapo Ijumaa," amesema Maalim Seif.
Social Plugin