Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wanaosogelea kituo cha polisi Nyakato wakidai kuwa kuna vichwa vya watoto takribani vine vimekamatwa leo.
Akizungumza na Malunde1 blog, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,ACP Jumanne Muliro amesema wananchi hao walikusanyika na kuanza kusogelea kituo cha polisi baada ya kutokea uvumi huo.
“Kimsingi ni uvumi ambao hauna msingi,watu wakajikusanya,sasa wanajikusanya wanasogelea kituo cha Polisi cha Nyakato wanasema kwamba vichwa vipo ndani,tunawaelewesha tukiwaambia hakuna vichwa wana hakuna kitu kama hicho,Hii nchi haiwezi kuendeshwa kwa uvumi mtu anaanzisha tu halafu watu wanakurupuka badala ya kufanya kazi za msingi”,amesema Kamanda Muliro.
“Kundi kubwa la watu linataka kusogelea kituo cha polisi ambacho kina dhana mbalimbali za kiusalama,sisi tunafanya jukumu la kuzuia,tulichofanya tulipiga mabomu machache ya machozi,watu wakatawanyika,tukawaambia hicho kitu wanachokisema hakipo...
“Pia tumefanya jukumu na kuanza kufuatilia ni nani alikuwa chanzo cha uvumi huo,kuna mtu mmoja tunamshikilia,tunamhoji atuambie alipata taarifa hizo wapi na watatu ambao walikuwa wanakaidi kutoka karibu na kituo cha polisi na wenyewe tunawahoji kwamba hayo mambo wameyapata wapi,hivyo kwa kifupi hali ni shwari”,ameongeza Muliro.
Social Plugin