MADURO AMUOMBA PAPA FRANCIS KUINGILIA MGOGORO VENEZUELA

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amemwandikia barua kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akimwomba kuingilia kati kwenye mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini mwake.

"Nimemwandikia barua Papa Francis, akisema kwamba anamwomba kiongozi huyo kusaidia kufanikisha mchakato wa majadiliano", alisema rais Maduro wakati akizungumza na kituo cha habari cha Italia cha SkyTg24. 

"Ninamuomba Papa kutusaidia, kwenye mchakato wa majadiliano. Ninatumai tutapata majibu ya kutia moyo kutoka kwake", aliongeza Maduro.

 Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa pamoja wamesema wana matumaini ya ufumbuzi wa amani kwenye mgogoro huo wa kisiasa, huku Merkel akisema taifa lake linamtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido aliyejitangazia mwenyewe kuwa rais wa mpito.

Merkel ambaye yuko ziara ya siku mbili nchini Japan, ameungana na mataifa mengine ya Ulaya, kumtambua Guaido kama rais wa mpito na kusema anapaswa kuandaa uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo. 

Waziri mkuu Abe, hata hivyo hakutoa msimamo juu ya Guaido, lakini alisema Japan inataka suluhisho la amani na demokrasia kwenye mgogoro huo.

Chanzo:Dw

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post