Mwanaume mmoja anashikiliwa na vyombo vya usalama nchini Malawi baada ya kukutwa akisafiri na maiti ya mtoto kwenye treni.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Joseph Sauka, amesema kwamba mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la James Majawa, 28, wa kijiji cha Chimphamba alikuwa akisafiri kutoka Limbe kwenda Nayuchi.
Kamanda Sauka ameeleza kwamba maiti ya Mtoto huyo ilibainika baada ya harufu ya kitu kilichoharibika kuenea kwenye Treni hiyo iliyokuwa na abiria wengine.
Amefafanua kwamba baada ya upekuzi ndipo maiti hiyo ikabainika huku ikiwa imetolewa sehemu za siri.
Hata hivyo Kamanda Sauka ameeleza kwamba bado wanaendelea na uchunguzi zaidi huku wakisisitiza kwamba maiti hiyo siyo ya mtoto mwenye ualbino.
Social Plugin