Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATATU WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MWANZA



Moja ya mwili aliyepigwa risasi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwaua majambazi watatu waliokuwa na silaha za moto na silaha za kijadi ambao walifika katika maeneo ya Nyakabungo, Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana kwaajili ya kufanya uhalifu wa kuvunja maduka ya wafanyabiashara.

Majambazi hao walifika katika mtaa huo kwa lengo la kuvunja maduka ya wafanyabiashara ndipo raia wema walipotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Askari Polisi waliokuwa doria baada ya kupata taarifa hizo walifika katika eneo la tukio na majambazi walipogundua uwepo wa askari katika eneo hilo walianza majibizano ya risasi ili kujihami.

Advera Bulimba ni Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza amethibitisha kuuawa kwa majambazi hao pamoja na kutoa wito kwa wananchi wanaofanya uhalifu mkoani humo kutojihusisha na matukio ya kihalifu.

Miili ya majambazi hao watatu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwanza Sekoutoure kwa ajili ya utambuzi.
Via>EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com