Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ameongoza shughuli za mazishi ya Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla yaliyofanyika leo Ijumaa Februari 22, 2019 saa kumi jioni katika kijiji cha Puge, Nzega vijijini jimboni kwa Waziri Kigwangalla.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri Wabunge pamoja na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Marehemu Zul alifikwa na mauti jana majira ya saa nne asubuhi JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akiwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.
#R.I.P Zul.
Inna lillahi wainna illaihi rajiuun
Social Plugin