Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKONDA ATOA MILIONI 5 KUMSAIDIA KIUCHUMI MAMA YAKE GODZILLA.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Tsh. Milioni 5 kwa Mama mzazi wa Godzilla kama sehemu ya kutimiza malengo ya marehemu aliyokuwa ameyaweka kwa mama yake kabla ya kukutwa na umauti.

RC Makonda ameeleza hilo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa mpendwa Godzilla inayofanyika katika viwanja vya Salasala Dar es Salaam.
"Ndugu yetu alikuwa na mipango wa kumsaidia mama yake kiuchumi, akawa amempa milioni nne lakini akawa na malengo ya kumpa milioni tano ili aweze kuanzisha famasi kama sehemu ya kujitengemea kiuchumi," amesema.

Amesema kuwa baada ya Godzilla kuanza kuumwa mama yake alitumia fedha hizo, hivyo yeye atatoa Milioni tano ili kumuwesha mama Godzilla.

RC Makonda amesema fedha hiyo atatoa siku ya Jumatano na msanii Fid Q ndio atakabidhiwa ili akamkabidhi mama yake Godzilla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com