Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMA MPENDA 'LIMBWATA' AAMBULIA TALAKA AKISAKA DAWA KWA SANGOMA MUME AMTII ZAIDI

 Mwanamke mmoja mwenyeji wa Kagumo, Kirinyaga nchini Kenya amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutemwa na mumewe kutokana mume huyo kubaini kuwa mkewe alikuwa akitafuta nguvu za giza kwa mganga wa jadi akitaka kudumisha mapenzi kati yao ili mumewe aweze kumpenda na kumtii zaidi.

 Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, mwanamke huyo aliamua kutafuta msaada wa mganga ili mapenzi yanoge na hata kupewa pesa nyingi na mumewe

 Inadaiwa kuwa licha ya kumlipa mganga huyo na kumtembelea mara kadhaa, lengo la mwanamke huyo halikufanikiwa.

 Siku ya kioja, mganga huyo ambaye alikuwa mnywaji wa pombe alikutana na mume wa mwanamke huyo kwenye baa, baada ya kubugia pombe na kulewa, alianza kumrushia mume huyo cheche za matusi huku akieleza kuhusu jinsi mkewe amekuwa akitafuta dawa za mapenzi 'Limbwata' kwake.

"Hata mkeo ni mteja wangu shupavu, hunitembelea kila mara kutafuta hirizi ya kunogesha mahaba kati yenu,’’ alisema.

 Jamaa huyo alikasirika mno lakini akapata njia ya kujizuia. ''Wajua kuwa ndoa zina changamoto kadhaa na wanawake hawakosi vituko,’’ alimjibu mganga huyo. 

Jamaa alipofika nyumbani alimfokea mkewe. "Kila ulichofanya gizani imebainika. Wewe na mganga mna uhusiano gani,’’ aliuliza kwa hasira.

Mwanamke huyo naye alimruka na kudai kuwa hamtoshelezi kimapenzi. ''Mume asiyemtosheleza mkewe unatarajia apelekwe wapi?,’’ alisema kwa dharau.

 "Mganga huyo anayekutosheleza nenda kwake moja kwa moja,’’ Jamaa huyo" alisema huku akimfurusha mkewe. 

Licha mwanamke huyo kumwomba msamaha, aligoma kumsamehe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com