Mshambuliaji machachari wa Manchester United Anthony Martial amesaini kandarasi mpya na Manchester United itakayombakisha katika uga wa Old Trafford mpaka Juni 2024.
Anthony Martial amefunga magoli 46 katika mechi 162 alizoichezea Manchester United.
Martial mwenye miaka 23, alijiunga na United kutoka Monaco Septemba 2015 kwa pauni milioni 36, lakini hakuwa na furaha klabuni hapo mwaka 2018 na kocha aliyepita Jose Mourinho alikuwa radhi kumuuza.
Mkataba wake mpya utamfanya asalie na Mashetani Wekundu mpaka atakapotimu miaka 29, na kuna kipengele kinachoruhusu mkataba huo kuongezwa kwa mwaka mmoja.
"Kwa umri wake, ana ubongo mzuri wa mpira, ambao, ukijumuishwa na kipaji chake cha kipekee kinamfanya awe mchezaji mwenye mustakabali mzuri kabisa,"
alisema kocha wa muda wa United Ole Gunnar Solskjaer.
Mwezi Juni, ajenti wa Martial alisema mteja wake alikuwa anataka kuhama, na Mourinho alikuwa radhi, lakini uongozi wa United ulizima jaribio hilo na wakafungua ukurasa mpya wa majadiliano.
Chanzo:Bbc
Social Plugin