Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka jeshi la polisi kwa kushirikiana na TCRA kuhakikisha mtu yoyote atakaye mtukana, kumdhihaki, ama kufanya uchochezi dhidi ya Rais Dkt John Magufuli achukuliwe hatua mara moja.
Akiongea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kangi amesema, "wanaomtukana Rais kuanzia sasa wasakwe popote pale walipo wakamatwe".
''Haiwezekani Rais akatukanwa, haiwezekani kabisa, iwe kwenye magroup ya WhatsApp, iwe kwenye ujumbe mfupi wa simu au blog na hata aina yoyote ya mawasiliano wachukuliwe hatua za kisheria'', amesisitiza.
SIKILIZA HAPA CHINI
SIKILIZA HAPA CHINI
Social Plugin