Moja ya mwili wa mtoto ambaye alikuwa ameuawa mkoani Njombe mapema wiki iliyopita
**
Wakati watoto saba wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wakiripotiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani Njombe, Askofu wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Mkoa wa Geita, Heryyabwana Majebere, amesema mauaji hayo yamezuka hivi sasa ikiwa ni kuelekea kwenye mdogo wa serikali za mitaa.
Kwa mujibu wa Askofu Heryyabwana Majebere, huenda wahusika wakubwa wa mauaji ya watoto ni viongozi wa serikali na vyama vya siasa ambao ndiyo wateja wakubwa wa waganga wa jadi.
Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalumu ya kuwaombea watoto hao wasio na hatia, Askofu Majebere amesema amepokea kwa masikitiko mauaji ya watoto yanayoendelea Mkoani Njombe huku akibainisha kuwa watoto wana haki ya msingi ya kulindwa.
kuhusu mauaji hayo kuhusishwa na imani za kishirikina, Askofu Majebere amesema serikali inapaswa kuchukua hatua kali kwa waganga watakaobainika kujihusisha na ramli.