Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amesema anahofia kutaja majina ya watu waliomtahadharisha kuhusu namna mazishi ya kifo chake namna yalivyopangwa kwa kuwa hataki watu hao wapitie matatizo ambayo yeye tayari amekwishapitia.
Akizungumza na watanzania waishio Marekani, Lissu amesema kwamba alipatiwa taarifa na watu ambao hana mashaka nao kwamba siku aliposhambuliwa ilipangwa kuwa akifa asipelekwe Dar es salaam wala bungeni bali apelekwe akazikwe kijijini kwao.
Lissu amesema kwamba ipo siku itafika na majina atayataja, na kwamba watu hao watakuwa salama kwa kuwa yeye tayari ameshanusurika risasi 16 na hataki watu wapitie yeye alipopitia.
"Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets".
Pamoja na hayo Lissu ameeleza kwamba yeye anamarafiki wengi ndani ya Chama Cha Mapinduzi lakini kitendo cha viongozi ndani ya chama hicho kushindwa kwenda kumuona ni kutokana na kikao walichokalishwa na kuonywa (pasipo kumtaja jina) kwamba wasishabikie tukio lililompata.
Chanzo - EATV