Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC SHINYANGA AKERWA WATUMISHI WA UMMA KUWATOLEA LUGHA MBAYA WANANCHI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Tinde

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewataka watumishi wa umma kuacha mara moja tabia ya kutoa kauli mbaya kwa wananchi na badala yake wawasikilize na kuwatatulia shida zao.

Mboneko ametoa kauli hiyo leo Februari 21,2019 wakati akisikiliza kero za wananchi wa kata ya Tinde ambapo alielezwa kuwa baadhi ya watumishi katika kituo cha afya Tinde wamekuwa wakiwatolea lugha chafu wananchi pindi wanapohitaji huduma kwenye kituo hicho.

Mkuu huyo alikemea vitendo hivyo akisema hatakubali kuona watumishi wa umma wakiwatolea lugha mbaya wananchi.

“Mimi kama kiongozi mkubwa wa serikali sitakubali watumishi wa serikali kuwatolea lugha mbaya wananchi,Mtumishi umeletwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,kama umeshindwa kufanya kazi ni vyema ukatupisha”,alisema.

“Wasikilizeni wananchi,endeleeni kuwahudumia vizuri,wapeni majibu wanayotaka badala ya kuwajibu ovyo”,aliongeza.

Mkuu huyo wa wilaya pia aliwakumbusha viongozi wa serikali za mitaa na kata kufanya mikutano ya hadhara na kusoma kusoma taarifa za mapato na matumizi.

Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kutowaozesha watoto wa kike na kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao shuleni ili kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kukua katika maadili mema.

“Ni vyema pia tukawapangia watoto wetu muda wa kurudi nyumbani,haiwezekani mzazi anarudi nyumbani saa 12 jioni halafu mtoto anarudi nyumbani saa nne usiku, mtoto anagonga mlango na wewe unanyuka kwenda kufungua..sasa hapo nani ndiye mzazi?”,alihoji Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Tinde - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akisalimiana na wazee wa Tinde kabla ya mkutano wa hadhara.
Mkazi wa Tinde Hassim Mkarambati akielezea kero ya majengo yaliyopo katika kituo cha afya Tinde kutotumika mpaka sasa
Masanja Saba akielezea kero ya maji Tinde
Mzee Mayunga akielezea kero yake kuhusu TANESCO kutowalipa na kufyeka mazao yao.
Said Diesel akielezea kero yake kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko
Hila Soudy akielezea kero yake kwenye mkutano
Yahya Baragash akielezea kero yake
Bernard Shimbi akielezea kero yake kuhusu upungufu wa walimu kwenye shule mbalimbali katika wilaya ya Shinyanga.
Pili Masunga akielezea kero yake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com