Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKENYA CLIFTON MIHESO ATUA ULAYA


Aliyekuwa winga wa Afc Leopards Mkenya Clifton Miheso amejiunga na klabu ya Ureno Clube Olimpico de Montijo.

Klabu hiyo ya Ureno imethibitisha kwamba imesajili mchezaji huyo wa Harambee stars ambaye alikuwa akiipigia Buildcon ya Zambia.

Klabu hiyo inasema Miheso ataongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ikumbukwe kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwa Miheso mwenye umri wa miaka ishirini na tano kupigia klabu ya Ulaya.

Klabu hiyo ya Olympic imetakia Miheso kila la heri klabuni hapo ambayo inapatikana mjini Montijo.

Montijo inacheza katika ligi ya daraja la tatu huko Ureno.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com