Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AJIUA DAR

Mtoto wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Msewe jijini Dar es Salaam, Daniel Mussa (10), anadaiwa kukutwa amejinyonga chumbani kwake nyumbani kwao Kimara Kona jijini.

Tukio hilo lililotokea Januari 30,2019 limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro, aliyedai uchunguzi wake bado unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

"Kuna mambo matatu hapo; kajinyonga, kafa au kauawa? Sisi bado tunachunguza ili kujua ukweli," Kamanda Muliro alisema.

Alisema hakuna mtu wanayemshikilia kutokana na tukio hilo, lakini wanafanya uchunguzi kwa watu wa karibu na mtoto huyo wakiwamo wazazi na ndugu zake.

"Sisi (Jeshi la Polisi) tunapochunguza, ninyi (waandishi wa habari) husema tunawashikilia, tunahoji watu wa karibu baba, baba mdogo na wengine ili kupata ukweli wa tukio," alisema.

Chanzo- Nipashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com