TAARIFA KWA UMMA
Tumepokea taarifa kutoka TANESCO, kuwa Tarehe 16 Februari, 2019 kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni watazima umeme kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la Chanzo cha Maji Capri-Point.
Kufuatia taarifa hiyo, tunasikitika kuwataarifu wateja wetu wote kuwa hakutakuwa na uzalishaji wa maji hadi hapo huduma ya nishati ya umeme itakaporejea katika hali yake ya kawaida.
Tunawashauri kutunza maji yatakayotosha katika kipindi hicho ambacho kutakuwa hakuna uzalishaji wa maji.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa mteja kwa namba 0800110023 (Bure).
Imetolewa Tarehe 15 Februari, 2019 na: -
OFISI YA UHUSIANO
MWAUWASA
Social Plugin