Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAULI YA MWIGULU NCHEMBA BAADA YA KURUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Mbunge wa Jimbo la Iramba, Mwigulu Nchemba ameruhusiwa kutoka hospitali hii leo kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatano, Februari 13,2019 mkoani Iringa.

Mbunge huyo alikuwa akisafiri kutoka Iringa kuelekea Dodoma, wakati gari lake lilipopata ajali hiyo katika eneo la Migori moani Iringa, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma.

Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao,

"Nashukuru Mungu nimeruhusiwa kutoka Hospitali, Shukran kwa mhe Rais na wasaidizi wake wote kwakuwa karibu nami,wabunge,viongozi wa Chama na Serikali, madaktari kwa matibabu ya haraka, wananchi wote kwa maombi yenu na salamu za kunitakia heri. Zaidi namshukuru Mungu kwa namna alivyonitetea mimi pamoja na dreva wangu, hakika kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa." 
(@mwigulunchemba) 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com