Watano wamefariki dunia leo Jumatano Februari 13, 2019 baada ya ndege ndogo waliyokuwa wanasafiria kuanguka katika kaunti ya Kericho nchini Kenya.
Ndege hiyo ilianguka kwenye msitu wa Londiani ikiwa na abiria watano, mkuu wa kikosi cha anga, Kamanda Rodgers Mbithi amesema abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki dunia.
Amesema waliopoteza maisha katika ndege hiyo Cesna 206-5-Y BSE ni wanaume watatu na wanawake wawili ambao hawajatambulika ni raia wa nchi gani.
Kwa mujibu wa kamanda wa kaunti ya Londiiani, Justus Munyao, ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Safari ambayo huchukua abiria kutoka Ol Kiombo kuelekea Kaunti ya Turkana.
Amesena tukio hilo lilitokea saa 5 asubuhi kwenye msitu wa Masaita.
Kamanda wa Kikosi cha Rift Valley, Edward Mwamburi amesema polisi wameshafika eneo la tukio.
Via Mwananchi
Social Plugin