Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KESI KUPINGA WAKURUGENZI KUSIMAMIA CHAGUZI; SERIKALI YAKWAMA KORTINI


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la serikali kwenye shauri la kupinga utaratibu wa kuteuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamaizi wa uchaguzi.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe ambapo leo tarehe 13 Februari 2019, mahakama imeelezea kuwa, waombaji wanahaki ya kisheria kufungua shauri hilo.

Awali serikali ilitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa sababu, waombaji hawakustahili kufika mahakamani na badala yake kwenda kulalamika kwenye utawala wa tume.

Tarehe ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo itatajwa saa nane mchana baada ya mahakama kurejea tena.

Bob Chacha Wange kupitia wakiliwa wake Fatma Karume amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na mkurugenzi wake.

Bob Chacha Wangwe amefungua kesi hiyo kikatiba baada ya kuamini kuwepo kwa udhaifu wa tume hiyo. Amedai kuwa, tume hiyo inaongozwa na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawaendishi uchaguzi wa haki.

Bob Chacha Wange ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe aliyewahi kuwa Mbunghe wa Tarime mjini (Chadema).

Chanzo - Mwanahalisi online 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com