Serikali imekamilisha upelelezi wa kesi ya kufanya ngono kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’ na mumewe Said Mtopali kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Leo tarehe 11 Februari Faraji Nguka, Wakili wa Serikali, ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile. Hata hivyo washtakiwa wamekana kufanya ngono kinyume na maumbile.
Wakili Nguka amedai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 7 Machi 2019.
Amber Ruth na mumewe walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Novemba 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mbali na wawili hao, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.
Katika kesi hiyo kosa la kufanya ngono kinyume cha maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa ametenda kati ama baada ya tarehe 25 Oktoba 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.
Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya 25 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam alifanya ngono na Amber Ruth kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.
Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya 25 Oktoba 2018 alisambaza video za ngono kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo WhatSapp.
Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati 25 Oktoba 2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii (Whatsapp). Kosa ambalo wamesema si kweli.
Chanzo- Mwanahalisionline
Social Plugin