Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa Huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa ajili ya kupatiwa Kitambulisho cha Taifa inatolewa BURE. Mwananchi anatakiwa kufika katika ofisi za NIDA akiwa na nakala (Photocopies) za viambatisho vyake muhimu.
Waombaji wote wa Vitambulisho vya Taifa mnakumbushwa kuwa “Rushwa ni Adui wa Haki. Usikubali kudai, kutoa wala kupokea Rushwa.” Kitambulisho cha Taifa ni haki yako ya msingi na hakiuzwi.
Hakikisha unahudumiwa katika Ofisi au Vituo rasmi vya Usajili vya NIDA na Afisa wa NIDA na sio Vishoka wanaojipenyeza kwenye zoezi.
Ukiombwa Rushwa Toa Taarifa kwa Mawasiliano :-
Simu: 0800758888 au 0673 333 444 au 0759102010 au 0765201020, Barua: S.L.P 12324 Dar es Salaam, Barua pepe (email): nida.tanzania@nida.go.tz. Tembelea tovuti yetu: www.nida.go.tz, Facebook nidatanzania, twitter @nidaTanzania au twitter.com/nidatanzania
Imetolewa na:- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Social Plugin