Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PAKA ARITHISHWA UTAJIRI WA BILIONI 456



Marehemu Karl Lagerfeld akiwa na Paka wake.

Paka aliyekuwa akimilikiwa na mkongwe wa mitindo Duniani marehemu Karl Lagerfeld ndie atakayerithi utajiri wote wa mkongwe huyo.

Paka huyo anayefahamika kwa jina la Choupette atamiliki utajiri wake ambao unatajwa kufikia zaidi ya shilingi Bilioni 456 za Kitanzania na inaripotiwa kuwa paka huyo alikuwa akilelewa kifahari na mmiliki wake tokea mwaka 2011.

Karl Lagerfeld alifariki Jumanne ya Februari 19,2019 jijini Paris akiwa na umri wa miaka 85 akiwa miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya pazia ya mafanikio ya nembo kama Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi mwaka 1980.

Umaarufu wa paka huyo umekuwa mkubwa hata katika mitandao ya kijamii, ambapo katika ukurasa wake wa Instagram unaoendeshwa na mtaalam wa masoko mitandaoni, Ashley Tschudin, umefikisha jumla ya wafuasi 120,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com