Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa kitika cha pauni £400,000 kwa wiki.
Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.
Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo.
Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka.
Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni £3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini.
Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa atasalia katika kumbu kumbu ya historia ya mashabiki.
Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa ataendelea kuwaunga mkono 100%".
"Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni." Aliandika Ramsey
Tovuti ya Juventus imemkaribisha Ramsey kwa kuandika kwamba atakuwa mkazi wa Wales wa tatu kuiwakilisha klabu hiyo baada ya John Charles na Ian Rush.
Chanzo:Bbc