Gharama za matibabu ya Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds TV na Redio, Ruge Mutahaba zimeelezwa kufikia zaidi ya Sh650 milioni hadi sasa huku kila siku akitumia kati ya Sh5 hadi Sh6 milioni.
Kwa muda sasa Ruge yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya figo na imeelezwa na mdogo wake, Mbaki Mutahaba kuwa kaka yake anaendelea vizuri.
Mbaki amesema mpaka sasa, Ruge ametumia kati ya Sh500 hadi Sh650 milioni kwa matibabu hayo na zaidi ya Sh530 milioni zimetolewa na Clouds Media.
Amesema gharama za matibabu ni kubwa lakini aliwashukuru watu mbalimbali wanaoendelea kujitolea kwa namna moja au nyingine.
Na Hellen Hartley, Mwananchi
Social Plugin