Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media group inayomiliki Clouds TV na Clouds Fm, Ruge Mutahaba amefariki dunia leo Jumanne Februari 26,2019 wakati akiendelea na matibabu nchini Afrika Kusini akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa miezi kadhaa.
R.I.P Ruge.Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) February 26, 2019
Social Plugin