Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kumchukulia hatua msanii, Godfrey Tumaini maarufu kama ‘Dudubaya’, kwa kumdhihaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, marehemu Ruge Mutahaba.
Mwakyembe ametoa agizo hilo leo tarehe 27 Februari 2019, baada ya Dudu Baya kusambaza video katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha akimdhihaki marehemu Ruge.
Tangu kutokea kwa taarifa za kifo cha Ruge jana, Dudubaya amekuwa akitoa maneno mtandaoni kumdhihaki Ruge akimtuhumu kuwa enzi za uhai wake alikuwa mnyonyaji wa wasanii.
Dudubaya amepost vipande vya video katika mtandao wa Instagram akimdhihaki Marehemu Ruge.
Aidha, Mwakyembe ameitaka BASATA kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua za kisheria Dudubaya kufuatia hatua yake hiyo.
Saa chache baada ya Mwakyembe kutoa agizo hilo, Dudubaya amemjibu akisema kuwa, bora mafuta yatakayotumika kwenye difenda kwenda kumkamata, bora yakakamate majambazi kwa kuwa yeye yuko tayari kwenda katika kituo chochote atakachoelekezwa na Jeshi la Polisi kwenda.
“Niko ‘home’ nyumbani mheshimiwa Mwakyembe umeagiza nikamatwe na jeshi la polisi, usisumbue madifenda kupoteza mafuta bora kakamate majambazi, waambie polisi waniite kituo gani kama ni Oysterbay, Salender Bridge, central au Mabatini ‘im raedy to come there, thisi is God is job,” amesema Dudubaya.
Social Plugin