Familia ya Ruge Mutahaba imetoa utaratibu wa mazishi ya ndugu yao, ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa Clouds Media Group, taarifa hizo zimetolewa na Ndugu Kashasha ambaye ni msemaji wa familia ya Ruge Mutahaba. Amesema kwamba kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa Ruge Mutahaba utafika Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya Ijumaa na iwapo ratiba itaenda sawa basi wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga siku ya Jumamosi katika viwanja vya Karimjee.
Baada ya hapo familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu.
Ruge amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49, huku akiwa mmoja wa waasisi wa Clouds Media Group
Social Plugin