Mkuu waKikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akimkabidhi koti la usalama barabarani(Reflectors) Michael mmoja wa madereva bodaboda mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL).
Kampeni hiyo inalenga kupunguza idadi ya ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akimkabidhi kifaa cha usalama barabarani (Reflectors) Yusuph Ramdhan ambaye ni dereva bodaboda mkoani humo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL). Kushotoni Mkuruugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akionyesha mfano wa makoti ya usalama barabarani (Reflectors) kwa ajiliyamaderevabodabodamkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL).Kampeni hiyo inalenga kupunguza idadi ya ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli akipeana mkono na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Unywaji kiistaarabu ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha” inayoratibiwa na Kampuni hiyo kwa lengo la kupunguza idadi ya ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini
Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni ya unywaji kiistarabu Mkoani Morogoro.
Morogoro, Februari 23, 2019– Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imeendelea na kampeni yake ya uelimishaji juu ya unywaji kiistarabu inayolenga kuwafikia wanafunzi wa vyuo,madereva, waendesha vyombo vya umma, na madereva bodaboda mkoani Morogoro.
Kampeni hiyo ya siku mbili ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto” itakayofanyika siku ya Jumamosi imelenga kuwafikia watu 1000 kupitia maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu za starehe ‘baa’, vyuo pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
Kampeni hiyo imezinduliwa Februari 23, 2019 katika Hoteli ya Nashera ambapo wadau mbalimbali wa usafirishaji ikiwamo Jeshi la Polisi, Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) na madereva walishiriki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugeni wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha kampeni hiyo imelenga kuwafikia watu 1,000 wakazi wa Mkoa huo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupunguza kiwango cha ajali za barabarani hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alisema kampuni hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwmao Jeshi la Polisi-kitengo cha Usalama Barabarani ambapo kampeni hiyo imekwisha kufanyika katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam mapema mwaka huu.
“Katika kampeni hii tunatoa vifaa mbalimbali vya uelimishaji ikiwamo vipeperushi, vibandiko (stika), makoti ya usalama (reflectors), fulana pamoja na kuwashirikisha wadau katika majadiliano yanayolenga katika kutokomeza baadhi ya mila na desturi potofu juu ya matumizi ya pombe,” alisema Wanyancha.
Aliongezaa“Unywaji kistaarabu hauishii tu katika kupunguza kiwango cha pombe bali ni kutokuruhusu pombe itawale maisha yako au iongoze mahusiano yako.”
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabrani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli aliishukuru SBL kwa jitihada hizo na kwamba kwa kulishirika Jeshi la Polisi ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya na kuzifanya barabara kuwa salama kwa watumiaji.
Hata hivyo, Deleli alisema anasikitishwa na vitendo vya baadhi ya madereva kunywa pombe kiholela pasipo kujali matokeo yake huku akitoa wito kuwa tabia hizo zinatakwa kukoma ili kupunguza ajali zinazowza kuepukika.
“Jeshi la Polisi, madereva, watembea kwa miguu na makampui kama hii ya Serengeti na jamii kwa ujumla tuna wajibu wakuhakikisha kuwa barabara zetu zinakuwa salama kwa kuhamasisha madereva kuzingatia unywaji kiistarabu,” alisema Deleli.
Aliongeza, “Nafarijika kuona kwamba licha kuwa ni Serengeti ni wazalishaji wa bia lakini wamejitoa kwaajili ya kupambana na tatizo la ulevi hasa kwa maadereva ambao wanabeba dhamana ya maisha ya watu wengi,” alisema Deleli.
Kuhusu SBL
Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko.
SBL inaendesha viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.
Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick.
SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.
……………………………………………………
Kwa habari zaidi wasiliana na:
John Wanyancha,
Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL
Simu: 0692148857
Imani Lwinga
Meneja wa Mawasiliano, SBL
Tel: 0785428282
Social Plugin