Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

COCA-COLA YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA SCHWEPPES +C


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa Coca Cola Kwanza Bw. Erastus Mtui akifatiwa na Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Coca Cola Kwanza Bi. Josephine Msalilwa, Mkurugenzi wa Logistics Bw. Pankaj Singh pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano na Matukio ya kijamii Bw. Haji Ally wakiwa kwenye Uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha Schweppes +C.
Maneja Masoko na mauzo wa kampuni ya Coca Cola Kwanza Bi. Josephine Msalilwa akielezea kuhusu ladha tamu ya Kinywaji Kipya cha Schweppes +C
Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, imezindua kinywaji kipya chenye ladha ya limao kinayojulikana kama Schweppes +C, ikiwa ni sehemu ya kuongeza machuguo ya bidhaa kwa wateja wakeKinywaji cha Schweppes +C kinawalenga zaidi wateja wenye umri mkubwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Basil Gadzios, alisema kampuni yake imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ugunduzi na kuongeza idadi ya bidhaa tofauti tofauti ikiwa na lenga la kukidhi mahitaji ya wateja tofauti tofauti katika soko la Tanzania.

Tunayofuraha kuongeza bidhaa nyingine mpya sokoni ikiwa ni shehemu ya jitihada za kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Schweppes +C yenye ladha ya limao inawaletea wateja wetu ladha ya kipekee ya limao ikiwa na Vitamini C ambayo tunaamini wataifurahia. Kinywaji kimetengenezwa mahsusi kumpa mtumiaji wake ladha nzuri ya juisi ya limao. Tukiwa kama kampuni ya vinywaji baridi, tumejidhatiti kuwaletea wateja wetu kilicho bora na bado tuna vingi kwa ajili yao, alisema mkurugenzi huyo.

Gadzios aliongeza kuwa, Coca-Cola inatarajia kuingiza sokoni bidhaa nyingine nyingi ambazo siyo tu zitakidhi mahitaji ya jamii ya leo bali pia zitaendana na wateja ambao mahitaji yao hubadilika katika soko la kileo huku akiongeza kuwa kinywaji hicho kipya kimetengenezwa kwa kuzingaatia viwaango vyaa kimataifa kikiwa na ladha ya kipekee ya limao.

“Kuwashirikisha wateja wetu, ni moja kati ya vipao mbele vya kampuni ya Coca-Cola. Hii inatusaidia kuyafahamu mahitaji yao ambayo hubadilikakulingana na muda na hivyo kutuwezesha kuwatengenezea bidhaa zinazoendana na mahitaji na matakwa yao kuwashirikisha.

Kuongezwa kwa Vitamin C kwenye kinywaji kipya cha Schweppes +C, kunakifanya kinywaji hiki kitofautiane na vinywaji vyetu vingine vilivyopo sokoni huku kikiwapa wateja ladha murua ya limao, alieleza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com