Serikali mkoa wa Songwe imetoa majeneza 19 kwa ajili ya kuhifadhia miili ya watu 19 waliofariki kwa ajali usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 22, 2019 katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Akizungumza leo, mkuu wa wilaya ya Mbozi, John Palingo amewaambia waombolezaji waliofika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Serikali ya mkoa wa Songwe (Vwawa) kuwa kazi ya kutambua miili hiyo inasimamishwa kwa muda ili kupisha wataalamu waiweke vizuri miili hiyo iliyoharibika vibaya.
“Serikali ya mkoa imetoa majeneza hayo ili kuweza kuistiri vizuri miili kisha baada ya hapo kazi ya kuitambua itaendelea kama kawaida,” amesema Palingo.
Social Plugin