TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika kipindi cha miezi kumi iliyopita
tangu kuchaguliwa kwa bodi mpya ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga
chini ya Mwenyekiti LUHENDE RICHARD LUHENDE,kimefanikiwa kupunguza wafanyakazi
takribani 12 na kulipwa stahiki zao.
Aidha kiasi cha Tshs 95,155,118.00
kimeweza kutumika kuwalipa watumishi hao.
Watumishi hao wamepunguzwa kama jitihada
za chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga
katika kujiimarisha kiutendaji na ni mkakakti endelevu wa Kupunguza na
kuwalipa stahiki zao watumishi ambao wamehudumu kwa muda mrefu katika chama
hicho.
Sambamba na hilo Bodi ya SHIRECU (1984)
ltd imeajiri menejimenti mpya ya wakuu wa idara za Uhasibu,Utumishi,Tehama na
Ukaguzi wa ndani ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika union.
Imetolewa na:
Idara ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano
Shinyanga Regional Cooperative Union
(SHIRECU(1984)LTD).
26.02.2019.
Social Plugin