Watu wawili wa familia moja, Zulfa Chami na Zuhura Chami wamepoteza maisha, baada ya kupigwa shoti ya umeme na kamba ya kuanikia nguo katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi.
Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadae kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamisi Issah zinaeleza kuwa ndugu hao wa familia moja walifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa shoti ya umeme.
"Ni kweli ni mtu na dada yake wamefariki dunia leo kati ya saa 3:00 na 3:30 asubuhi katika eneo la Pasua Manispaa ya Moshi", amesema Kamanda Issah.
Chanzo - Nipashe
Social Plugin