Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MWANZA MGENI RASMI MKUTANO WA WANAMUZIKI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano utakao wakutanisha Wanamuziki wa fani mbalimbali waliopo jijini Mwanza.

Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga (pichani) alisema mbali ya Mongela kuwa mgeni rasmi pia kutakuwa na Mbunge wa Kiteto, Mheshimiwa Koshuma ambaye atakuwa mgeni maalumu.

Akizungumzia mkutano huo Dk.Kisanga alisema ni wa muhimu sana kwa wanamuziki hao kwani kutakuwepo na fursa nyingi.

"Mkutano huu utakaofanyika New Mwanza Hoteli ni wa muhimu sana hivyo nawaomba wanamuziki mbalimbali kufika kwani ni fursa ya pekee" alisema Kisanga.

Kisanga alisema mkutano huo umejaa fursa mbalimbali na kuwa TAMUFO imezialika taasisi mbalimbali ili kuelezea fursa walizonazo ili kuboresha maisha ya wanamuziki.

Alisema kwamba maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com