Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri, amesema hatakuwa kizingiti kwa Eden Hazard ikiwa nyota huyo wa miaka 28 ataamua kujiunga na miamba wa ujispania Real Madrid msimu ujao. (Star)
Lakini Cesc Fabregas anaamini Hazard huenda akasaini mkataba mwingine na Chelsea katika hatua ambayo itakomesha tetesi kuhusu uhamisho wako. (Independent)
Tottenham wanajiandaa kuweka dau la pauni milioni 35 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 20, licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mahasimu wao katika ligi ya Uingereza, Liverpool. (Daily Express)
Manchester Unitedwanatarajiwa kuminyana na mahacimu wao Manchester City kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, 22 msimu ujao. (Mirror)
Tanguy Ndombele (kushoto) aliisaidia Lyon kushinda Manchester City katika ligi ya mabingwa mwezi uliyopita
Vilabu vya Chelsea, Manchester United na Liverpool vinapania kumnunua nyota wa Benfica Joao Felix, 19. (Talksport)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali tetesi kuwa klabu hiyo itatumia fedha nyingi msimu ujao kuwasajili wachezaji wapya. (Teamtalk)
Kipa David de Gea, 28, anakaribia kutia saini kandarasi ya miaka mitano na klabu ya Manchester United. (Metro)
Chanzo:Bbc
Social Plugin